Karibu tena katika jikoni kulikoni. Jikoni leo tutapika
rosti la viazi mbatata na samaki wa kukaanga . mlo huu watu wengi uupika lakini
leo tutapika tofauti kidogo na tupikavyo majumbani kwetu ili kupata ujuzi mwingine wa kupika
chakula hiki na kupata radha tofauti na tamu kuliko unayopata siku zote.
Mahitaji ya rosti ya viazi mbatata
- Viazi mbatata ¼
- Nyanya maji 3
- Kitunguu maji 1
- Kitunguuu swaumu kijiko 1
- Binzari ya pilau ½ kijiko
- Mdalasini ½ kijiko
- Nyanya ya kopo 1
- Pilipili mboga/kuwasha
- Karoti na hoho 1
- Chumvi kiasi
- Limau 1
- Mafuta ½ chupa
Jnsi ya kuandaa rosti la viazi mbatata
- Menya viazi na katakata vipande vidogo vidogo na kuvisafisha vizuri kwenye chombo safi, kisha anza kusafisha nyanya karoti, vitunguu na karoti. Andaaa vitunguu swaumu kwa kuvimenya na kuviponda,kisha katakata vitunguu maji na nyanya .
- Chukua kiaangio Kaanga viazi vikiiva weka pembeni, katika sufuria kaanga vitunguu maji hadi viwe vya kawahia weka pilpili mboga/kuwasha na karoti.
- Kaanga vikikaribia kuiva weka nyanya maji kaanga vizuri hadi ziive, weka nyanya ya kopo na limau kiasi ila usisahau kuweka chumvi.
- Ikisha iva, changanya na viazi ulivyovikaanga na rosti, uku ukiendelea kuvichanganya taratibu, hakikisha viazi avirojeki sana.
Mahitaji ya samaki
- Samaki 1
- Pilipili manga/mtama ½ kijiko
- Tangawizi ½ kijiko
- Kitunguu swaumu
- Chumvi kiasi
Jinsi ya kuandaa samaki
- Safisha samaki kwa maji safi, kuondoa magamba na vitu vya tumboni na mapezi
- Muweke viungo kwa kupaka sehemu zote kwa kumpaka pilipili, tangawizi, kitunguu swaumu pamoja na chumvi, subiri kwa muda wa dakika 30 viungo vikolee kwenye samaki wako.
- Weka kikaangio mafuta, mafuta yakisha pata moto, kaanga samaki uku baada ya muda unamgeuza upande wa pili.