Wednesday, 15 April 2015

CHAPATI ZA MAZIWA



Jikoni kulikoni tutakuwa tunazungumzia maswala ya jikoni hasa uandaaji,na  jinsi ya kupika vyakula katika hali ya  usafi. Tutapika vyakula mbalimbali. Lengo kuelimisha jamii juu ya kupika vyakula,na usafi wakati tunaandaa na kupika kwasababu vyakula vina umuhimu wake katika mwili wa binadamu. 

Leo nakukaribisha katika dondoo ya upishi ambapo leo nitaelezea namna ya kupika chapati za kumimina hivyo basi ingawa watu wengi wamezoea kupika chapati hizi kwa kutumia maji lakini leo tutaandaa chapati hizi kwa kutumia maziwa

Mahitaji
  • Unga wa ngano ½ kilo
  • Mayai 4 maziwa ya kutosha 
  • Chumvi kijiko cha chakula 
  • Tangawizi ya unga kijiko kimoja cha chai 
  • Vitunguu maji, hoho, na karoti 
  • Mafuta.
Hoho na karoti
Vitunguu
Mafuta
Tangawizi ya unga

Chumvi

Maziwa
Ngano



Mayai



Njia 
  1.  Kwanza kabisa chekecha unga kwa aajili ya kuondoa uchafu na pumba.  
  2. Weka unga wako katika unga safi, changanya unga ,tangawizi pamoja na chumvi au sukari kwa wale wanaopenda kuweka sukari kwenye chapati za kumimina. 
  3. Sugua vitunguu maji kama unavyo sugua karoti upate vijiko viwili vya chakula au kata vipande vidogo vidogo, Andaa mayai katika bakuli linguine piga mayai.
  4. Anza kuchanganya mchanganyiko wako wote wa mayai, karoti, hoho, vitunguu na maziwa kwenye unga uliouandaa uku ukikologa hadi pate mchanganyiko laini . 
  5. Endelea kuchanganya hadi vitunguu viachane na kupotelea kwenye unga, hakikisha vitunguu havitoi mabonge, ongeza au maziwa kama mchanganyiko wako bado mzito hadi upate mchanganyiko mwepesi.
  6. Weka kikaangio kwenye moto.Tia mafuta kidogo tu, na yapashe moto.
  7. Chota mchanganyiko kijiko kikubwa, tandaza vizuri kwenye kikaangio, acha iive mpaka inapata rangi ya kahawia. Geuza upande wa pili na kuongeza mafuta kidogo uku ukiendelea kuigeuza geuza na iache mpaka iive.Ondoa na weka kwenye sahani safi na ufunike. 
  8.  Endelea kufanya hivyo mpaka mchanganyiko wote wa unga unaisha.

Chapati za maziwa

Hapo chapati zako zitakuwa tayari kwa kuliwa, unaweza kula.chakula hiki kizuri huliwa hasa kwa nyakati za asubuhi kwa ajili ya kufungua kinywa. Pia unaweza kula  jioni au usiku, unaweza kula kwa supu au mchuzi wa nyama au samaki. Pia unaweza kula kwa kushushia na chai, soda, juisi au maji.




5 comments:

  1. yamyam pishi zuri sana asante kwa dondoo nzuri umeniongezea ratiba ya mapishi nyumbani kwangu

    ReplyDelete
    Replies
    1. usijali farida utajua mengi na utaweza kubadilisha ratiba za vyakula nyumban kupitia jikon kulikon

      Delete
  2. Mh!! best hizo chapati za mayai me huku hoii.. umenikosha niajeee....

    ReplyDelete