Friday, 17 April 2015

kisamvu cha nazi



Naaam leo katika jikon leo tutaandaa kisamvu cha nazi, kwanza kabisa napenda kukueleza ya kuwa mboga za majani zinahitajika mwilini kwa sababu zina aina nyingi za  madini  na vitamini, hasa vitamini A na C vitu ambavyo ni vya lazima katika kukuza na kulinda mwili usipatwe na maradhi.

 Pia husaidia chakula kuyeyushwa haraka tumboni. Jikon leo tutaandaa kisamvu cha nazi na unashauriwa kupika mboga za majani mara baada ya kuzichuma. 

 Mahitaji
kisamvu

chumvi





nazi
kitunguu
kitunguu swaumu



 Njia
1.      Chambua kisamvu, kisafishe vizuri kwa maji na chumvi ilikuondoa uchafu na wadudu, na ukitwange kwenye kinu ukichanganya na vitunguu swaumu mpaka kiwe laini, kuna nazi na uchuje tui zito (tui bubu) na jepesi.

2.      Anza kuchemsha kisamvu,uku ukiendelea kutayarisha viungo. Katakata kitunguu maji, hoho na karoti, kisamvu kikishaanza kuiva na maji kukauka, weka kitunguu,hoho, karoti na chumvi.kisha weka tui jepesi ili kiendelee kuiva na kuwa laini zaidi 
3.      Tui likikauka weka tui zito pika hadi tui likauke kabisa hapo ndo utaona utamu wa kisamvu.
4.      Kisamvu hiki kinaweza kuliwa na wali au ugali, kisamvu ni mboga inayotupatia virutubiho na madini mwilini lakini kisamvu hicho hicho  kikiwa shambani mti wake ni kuni, mizizi yake unaweza ukapata unga wa ugali, muhogo unaweza kupika  ikawa kitafunwa ama kifungua kinywa kwa kushushia na chai, maji vilevile unaweza kupika uji wa mhogo.



5.     Jiandae  na kwa mapishi ya mbogamboga mchanganyiko. Usichoke endelea kusoma blog hii ili kujua mambo mengi zaidi kuhusiana na vyakula.

No comments:

Post a Comment