Monday 20 April 2015

MCHANGANYIKO WA MAHARAGE MAKAVU NA NYAMA


Kama ilivyo ada kila siku tunahitaji kufahamu kilichpo jiikoni. Jikoni leo tumeandaa mchanganyiko wa maharage na nyama. Nyama na maharage  ni aina ya protini ambayo hujenga mwili wa binadamu, vilevile nyama hutupatia vitamini B, chuma, fosiforasi na mafuta.
Maharage pia ni aina ya chakula jamii ya wanga,Ili kuweza kuhakikisha kwamba mwili umepata kiasi cha kutosheleza cha protini kwa siku ni vizuri kuchanganya maharage na nyama.
Jambo hili lina maana sana kwa sababu protini iliyoko katika maharage sio kamili inaweza kukamilishwa kwa kuchanganywan na vyakula vingine vyenye asili ya nyama. Ili mchanganyiko wako uwe mtamu, unatakiwa kupikwa vizuri na mapishi yabadilike siku hadi siku.

Mahitaji
  • Maharage makavu kikombe cha chai 1
  • Nyama bila mfupa ¼ kilo
  • Vitunguu maji
  • Nyanya kubwa za kuiva 3
  • Binzari au viungo vya mchuzi kijiko 1
  • Mafuta kijiko cha chakula 2
  • Pilipili ukipenda
  • Hoho na karoti
  • Limau 1
Njia

  1. Chagua maharage, safisha na kuyaloweka kwa muda wa masaa matatu
  2. Baada ya kuloweka maharage yako. Pika maharage kwa maji yale yale uliyolowekea mpaka yalainike.
  3. Osha nyama ikatekate vipande vidogo vidogo, weka maji ya limau au ndimu.
  4. Katakata vitunguu, hoho, karoti na nyanya. Kaanga vitunguu, hoho na karoti kisha weka nyama na kaanga. Ongeza  nyanya, chumvi,pilipili, na viungo vya mchuzi, endelea kupika mpaka nyama iive
  5. Nyama ikisha iva weka maharage yaliyoiva bila maji, koroga na kupika kwa muda mfupi.
  6. Ongeza maji ya kutosha ili kufanya mchuzi uwe mzito. Acha ichemke kwa muda mfupi.
  7. Tayari mboga yako itakuwa immeiva pakuwa na waweza kula mboga hiyo kwa ugali au wali  ili mlo wako ukamilike ni lazima uwe na mboga mboga za majani pembeni au matunda
wali na mchanganyiko wa maharage na nyama

No comments:

Post a Comment